Recent Posts

UJIO WA VIONGOZI KUTOKA OFSI YA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA
Tarehe 02/03/2023 Shirika la Green Community Initiatives tulipata wageni kutoka ofsi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga (serikali ya mkoa). Ujio huu wa wageni uliambatana na mazungumzo tuliyoyafanya ofsini (Ofsi ya GCI). Miongoni mwa wageni hao waliotutembelea alikuwemo Bwana Ngwale (Afsa Maendeleo Mkoa) na Bi Aisha Omary (Afsa Maendeleo wa wilaya).

Mazungumzo hayo yalijumuisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa mradi wa ACHA UKATILI tulioutekelezeka kwa kata za Lyamidati, Itwangi na Nsalala. Miongoni mwa taarifa tulizowasilisha serikalini ni pamoja na namna tulivyokuwa tukitekeleza, changamoto tulizokumbana nazo pamoja na mafanikio tuliyoyafikia ikiwemo uibuaji wa kesi pamoja na utatuzi wake. Vile vile tuliweza kutoa ushauri juu ya kipi kifanyike ili kuboresha utendaji kazi wa wadau kwa kushirikiana na serikali kwa ngazi za Kijiji hadi wilaya.