Recent Posts

Kupitia Mradi wa Urithi Wetu PTP-II shirika la GCI laendelea na shughuli za Uhamasishaji na utoaji wa elimu ya kupanda miti, kutunza Mazingira, Misitu na Historia ya Tanzania Mkoa wa Kigoma katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji

Leo tarehe 22/01/2025, Shirika la Green Community Initiatives (GCI) na shirika la APHI Foundation kwa kushirikiana na asasi mbalimbali chini ya Mtandao wa Urithi Wetu, kupitia Mradi wa Urithi Wetu (PTP - II), limeendelea kutekeleza shughuli za utunzaji wa mazingira, misitu, na kuhifadhi historia ya Tanzania katika Manispaa ya Kigoma Ujiji. Shughuli hizi zinafanyika kwa kushirikisha taasisi ya Misitu Tanzania yaani Tanzania Forest Services {TFS} ofisi ya Mkoa wa Kigoma.

???? Siku ya leo Jumatano, jumla ya miche 230 ya miti ya asilia na ya matunda imepandwa katika Kata tatu:

✅ Kata ya Kitongoni:

  •  Zahanati ya Kitongoni {Miche 25} 
  •  Shule ya Sekondari Kitongoni {Miche 25}

✅ Kata ya Mwanga Kusini:

  •  Ofisi ya Mtendaji wa Kata {Miche 8}
  •  Shule ya Msingi Muungano {Miche 58}

✅ Kata ya Kagera:

  •  Shule ya Msingi Kagera {Miche 60}
  •  Shule ya Sekondari Wakulima {Miche 58}

Kando na shughuli za upandaji miti, tumetoa elimu ya utunzaji wa mazingira na kuhamasisha jamii kushiriki kwenye matembezi ya hisani yatakayofanyika kutoka Kigoma Ujiji hadi Zanzibar Kizimkazi. Matembezi haya, yanayopitia njia ya watumwa {• Kigoma Ujiji, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Dar es salaam, Zanzibar-Kizimkazi}, yanalenga kuenzi historia, tamaduni, na maeneo ya kihistoria ya Tanzania kwa vizazi vijavyo.

Pamoja, tunaweza kuhifadhi mazingira na urithi wetu wa kihistoria!