Recent Posts

Acha Ukatili Project: Uchechemzi wa kuondokana na Mila na Desturi Kandamizi zinazochangia uwepo wa Ukatili dhidi ya wanawake na watoto ndani ya jamii

Katika kuendeleza utekelezaji wa Mradi wa Acha Ukatili 2024 Uliofadhiriwa na WOMEN FUND TANZANIA TRUST (WFT-T)

Leo asubuhi, Green Community Initiatives iliongoza mdahalo wa kusisimua na wanamabadiriko ngazi ya jamii katika kata ya Nsalala. Mdahalo ulifanyika katika ukumbi wa ofisi ya kata, ambapo wajumbe walijadili kwa kina kuhusu mila na desturi nzuri zinazoweza kuleta mabadiliko chanya katika jamii na hivyo kutokomeza ukatili.

"Wanamabadiriko ngazi ya jamii walisema: 'Ni lazima tuchukue hatua madhubuti kubadili mila na desturi zilizochangia katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Lazima tuchochee mabadiliko chanya na kukuza ushirikiano wa kijamii ili kujenga jamii yenye haki na usawa,'" alieleza mmoja wa washiriki.

Washiriki walifikia muafaka kuhusu umuhimu wa kusonga mbele na harakati za kuchambua na kubadilisha mila na desturi zilizochangia katika ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Walisisitiza umuhimu wa kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi na badala yake kukuza ushirikiano na ushiriki wa wanawake na watoto ndani ya familia na jamii.

 

"Ni wajibu wetu kama wanajamii kuelimisha na kusaidia katika kuvunja minyororo ya mila na desturi kandamizi ambazo zimekuwa chanzo cha ukatili. Tunapaswa kushirikiana ili kuunda jamii salama na yenye usawa kwa kila mwanachama," alisema mmoja wa wazee wa kitongoji.

Alasiri ilipowadia, jitihada za Green Community Initiatives zilihamia katika kitongoji cha Shigangama katika kijiji cha Nshishinulu, kata ya Nsalala. Hapa, shirika liliongoza mdahalo wa kusisimua kati ya wazee na vijana katika VIJIWE VYA KAHAWA.

"Tunahitaji kuwa mabingwa wa mabadiliko katika jamii yetu. Lazima tujifunze kuhamasisha ushirikiano ndani ya familia na kuelimisha kuhusu umuhimu wa kuvunja minyororo ya mila kandamizi,'" alieleza mmoja wa washiriki wa mdahalo.

Kwa furaha, wanakijiji hao walifikia maamuzi ya kuwa mabingwa wa mabadiliko ngazi ya kitongoji na kijiji. Walikubaliana kuhamasisha ushirikiano ndani ya familia na kusisitiza umuhimu wa kuelimisha jamii ili kuvunja minyororo ya mila kandamizi.

Matukio haya mazuri yanathibitisha azma ya Green Community Initiatives katika kupigania haki na ustawi wa wanawake na watoto, na tunajivunia kuwa sehemu ya mchakato huu wa mabadiliko katika jamii.