Recent Posts

Shirika la Green Community Initiatives la fanya maadhimisho ya mtoto wa Afrika Wilaya ya Shinyanga

Shirika la Green Community Initiatives lafanya maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika kwa ngazi ya Wilaya (Wilaya ya Shinyanga vijijini) Maadhimisho haya yamefanyika leo tarehe 14/06/2023 katika kata ya Mwalukwa iliyoko Wilaya ya Shinyanga Vijijini.

Kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaofanya shughuli za ulinzi wa mtoto Wilaya ya Shinyanga vijijini wakiwemo ICS, RAFIKI SDO, TAI, ADD, OPE, TIDO pamoja na NELICO, Tumeweza kufanya mdahalo uliojumuisha wadau wa taasisi binafsi, serikali pamoja na wanainchi wa kata ya Mwalukwa.

Maadhimisho haya yaliambatana na utoaji wa elimu ya malezi na makuzi ya mtoto, elimu ya usalama wa mtoto, vilevile elimu ya kupinga ukatili dhidi ya watoto na wanawake.

Vilevile Maadhimisho yalikuwa na mdahalo ulioendeshwa na kusimamiwa na Meneja wa shirika la ICS Bi. Sabrina Majikata, mdahalo ulilenga sana mambo ya usalama wa mtoto katika ulimwengu wa KIDIGITALI

Mdahalo huu uliweza kutoa muda wa watoto kutoa hoja zao ikiwepo faida walizopata kutoka kwa taasisi binafsi (NGOs) hasa katika kuimarisha usalama na ulinzi baina yao, pamoja na changamoto mbalimbali zinazowakabili, pia watoto walisema ushauri wao kwa wazazi wao pamoja na kwa watoto wao wenyewe ikiwemo kutekeleza wajibu wao ili haki zao ziendelee kufanyiwa kazi ipasavyo.

Vilevile wananzengo walitoa maoni yao na vitu mbalimbali vinavyofanyika katika familia ambavyo vinachangia kuathiri malezi na makuzi ya mtoto hasa kuwepo kwa ukatili wa kijinsia katika masuala ya elimu (mtoto wa kike kukosa elimu kisa waolewe).

Baada ya Maadhimisho kwa kushirikiana na wadau wote tumetoa zawadi kwa watoto wa shule zote zilizopo kata ya Mwalukwa. Lengo la zawadi hizi ni kuwawezesha watoto wenye mazingira magumu na wenye mahitaji waweze kusoma vizuri shuleni. Miongoni mwa zawadi zilizotolewa ni Peds, Pen, Pencil, na Madaftari.