Shirika la Green Community Initiatives - GCI lashiriki maonyesho ya taasisi binafsi mkoani Shinyanga (NacCoNGO) yaliyofanyika ndani ya siku 3 kuanzia tarehe 08/06/2023 hadi 10/06/2023.
Maonyesho haya yalikuwa na KAULIMBIU YA MAONYESHO: Kukuza athari: Kuadhimisha Jukumu la NGOs katika kuwezesha jamii kwa Maendeleo endelevu.
MALENGO YA MAONYESHO HAYA:
- Kutambua michango ya wadau yaani NGO katika kuleta Maendeleo endelevu ndani ya mkoa wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla.
- Kuimarisha mahusiano na taasisi nyingine zinazoingiliana na NGOs zikiwepo taasisi za kifedha: CRDB, NBC, TRA pamoja na NSSF.
- Kushukuru na kutoa pongezi kwa wadau waliofanya vizuri katika maeneo mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli zake ndani ya mkoa wa Shinyanga ndani ya mwaka 2022.
Pia maonyesho haya yaliambatana sana na utoaji wa elimu hasa katika maeneo haya matatu yafuatayo:-
- Jinsi ya kuzuia ufadhili wa kigaidi pamoja na kuangazia masuala ya utakatishaji fedha
- Mafunzo ya matumizi ya NSSF kwa waajiri na waajiriwa ndani ya NGO
- Mafunzo ya TRA (Online Compliance)
Vilevile kikao kiliambatana na utoaji wa elimu na ushauri jinsi ya kuendeleza maendeleo ya NGO kwa kushirikiana na taasisi nyingine za kifedha hususani NSSF, TRA, CRDB na NBC