Recent Posts

MDAHALO WA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

TAREHE 01st FEBRUARI 2023

TUKIENDELEA KUTEKELEZA MRADI WA ACHA UKATILI :- tumeendeleakutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanainchi wa kijiji cha Nshihinulu kata ya Nsalala wakiwemo VIONGOZI WA VITONGOJI, KAMANDA WA SUNGU SUNGUWAZEE WA MILA, WAZEE WA JADI NA WAZEE WA NZENGO.

Tumeweza kuzungumza na wanakijiji hao tukatoa elimu ya ukatili wa kijinsia huku na wao wakitoa hoja zao za uelewa juu ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya wanawake na watoto. Kupitia majadiliano/mazungumzo hayo wanainchi hao wameahidi kuwa wataenda kuwa chachu na mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia ndani ya jamii ya kijiji cha Nshishinulu na kata kwa ujumla. Huku serikali ya kijiji ikiahidi kushirikiana nao bega kwa bega ili kuhakikisha ukatili wa kijinsia wanautokomeza kabisa ndani ya kijiji kwa malika yote yaliyopo kijijini hapo.

Akizungumza na wanainchi hao Meneja wa shirika Bwana Ngolelwa Masanja amesema ''Kama watu wote hawa mliopokea elimu hii mkaitumia vizuri mkizungumza na kuelimisha jamii kuanzia katika familia zenu, hakika motokeo ya kupinga ukatili kijijini hapa yatakuwa makubwa sana na kwa ujumla tutajenga jamii yenye mitazamo chanya kwa kila jinsi (me na ke) huku mkichochea maendeleo ya kijamii ndani ya kijiji na kata kwa ujumla"  Vile vile amewataka wanakijiji hao wakawe mstari wa mbele kuonesha mabadiliko muda wote watakaokuwa wakitekeleza majukumu yao ya kila siku kwa kujali jinsi na kila rika pasina vielelezo vyovyote vya ukatili wa aina yeyote ile.