Recent Posts

GCI Yashiriki warsha ya Tathmini Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto

Leo Tarehe 19/06/2024, Shirika la GCI limeshiriki kikao muhimu kilichozungumzia mchakato wa tathmini ya utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Maendeleo Malezi na Makuzi ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) kwa mkoa wa Shinyanga. 

Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Vigmarck Hotel uliopo Shinyanga Manispaa, huku kikijikita katika kuangazia mbinu bora ikiwemo ushiriki na ushirikishwaji wa wadau katika kutia nguvu ya utekelezaji wa Programu hiyo inayolenga kusaidia watoto walioko kati ya mwaka 0 hadi 8

Wadau kwa kushirikiana na serikali Halmashauri ya Manispaa na Mkoa wamejadili mengi yakilenga kuboresha Mazingira na utekelezaji bora wa Programu hiyo Mkoani Shinyanga.