Recent Posts

MAJADILIANO NA WANAKIJIJI WA KATA YA ITWANGI

Kwa kushirikiana na POLISI WA KATA, Shirika limeendelea kutoa elimu ya kupinga mila na desturi gandamizi zinazopelekea kuwepo kwa ukatili dhidi ya watoto na wanawake mkoani Shinyanga kata ya Itwangi kwa vijiji vya Butini, Zobogo, Itwangi na Kidanda.

Wanainchi wa kata hiyo wameahidi kuonesha ushirikiano wao na viongozi wao pamoja na jeshi la polisi ndani ya kata kuhakikisha watakapopokea taarifa au kuona wataripoti ngazi zenye mamlaka ya kushughulikia matukio ya ukatili aidha kwa viongozi wao wa serikali ya mtaa au kwa jeshi la polisi katani pamoja na mamlaka zingine zinazojihusisha na kupinga ukatili dhidi ya watoto na wanawake mkoani Shinyanga.

Akizungumza na wanainchi hao AFSA WA POLISI LA KATA, amewaomba wanainchi kuonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio ya aina yeyote yakiwemo ya ukatili unaotanyika ndani ya kaya na ndani ya jamii. Vile vile Afsa polisi huyo amawaomba wanainchi hao wasiwe na wasiwasi juu ya utoaji wa taarifa au kuogopa kutoa taarifa kwa mamlaka zinazohusika likiwemo jeshi la polisi katani.